(ABNA24.com) Rais Rouhani amesema hayo leo katika kikao na baraza lake la mawaziri na kusisitiza kwamba, wananchi wa Iran kwa kudumisha umoja na mshikamano wao watawaonyesha Wamarekani kwamba, wana nguvu na uwezo mkubwa.
Rais Hassan Rouhani amesema pia kuwa, Majlisi ya Ushauri wa Kiislamu (Bunge) ni chombo chenye nguvu nchini Iran na akaongeza kusema kwamba, mahudhurio yenye hamasa ya wananchi wa taifa hili katika uchaguzi wa Bunge Ijumaa ijayo kwa mara nyingine tena yatawakatisha tamaa maadui.
Rais wa Iran amesisitiza kuwa, sera za Marekani katika eneo la Asia Magharibi hususan kuhusiana na Iran ni mbovu na ghalati. Rais Rouhani amewakumbusha viongozi wa Marekani na kuwaasa akiwaambia, siasa za mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa hazifui dafu mbele ya umoja na nguvu ya wananchi wa Iran hivyo hawana budi kusalimu mbele mbele ya taifa hili.
Ijumaa ijayo wananchi wa Iran waliotimiza masharti ya kupiga kura watajitokeza katika majimbo 208 ya uchaguzi kwa ajili ya kuwachagua wabunge 290 wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu. Siku hiyo kutafanyika pia uchaguzi mdogo wa Baraza la Tano la Wanazuoni Wataalamu wa Kumchagua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi katika majimbo matano ya Tehran, Fars, Khorasan ya Kaskazini, Khorasan ya Razavi na Qum.
.............
340